Swahilinux Ni Nini?

Swahilinux ni mradi wazi unaolenga kuunda mfumo wa tarakilishi utakaotumia lugha ya Kiswahili.
Mfumo huu wa tarakilishi unatumia nguvu ya kernel maarufu ya Linux inayohakikisha kuwa mtumiaji anapata mfumo unaovutia na wenye usalama wa kutosha
Faili za tafsiri zimehifadhiwa kwenye repo yetu ya GitHub ambapo unaweza kuzipakua, kubuni tafsiri na kuturejeshea ili tuweze kupiga chapa nakala yako ikiwa itakubalika.

image

Chapisha Nyaraka

Unakaribishwa
Unaweza kusaidia kwa kutayarisha nyaraka zinazoeleweka za programu au mfumo huu. Uwepo wa nyaraka husaidia kufuatilia huduma zote na inaboresha ubora wa programu. Makini yake kuu ni maendeleo, uvumbuzi na ushiriki wa maarifa kwa wavumbuzi wengine.
image

Vumbua/Buni

Unaruhusiwa
Umepewa haki ya kusoma, kubadilisha, na kusambaza mfumo huu kwa mtu yeyote na kwa sababu zozote ilivyotajwa katika leseni ya umma ya GNU.
image

Zungumza Nasi

Utangamano
Unaruhusiwa kuwasiliana na timu ya usimamizi kutumia mitandao ya Gumzo, WhatsApp, Telegram, Facebook, na IRC.
Tunakurai pia kusaidia katika usambazaji wa taarifa za kweli toka kwa blog au njia zingine zozote zinazotumika na Swahilinux ili kuwasilisha taarifa.

Wasimamizi

profile

Swahilinux Microsystem ni daraja kati ya elimu, teknolojia na maendeleo. Ikiwa tunatamani kufanikiwa kwenye miisho yetu ya siku zijazo, inatubidi kubadili jinsi tunavyofanya kazi na kuamini kuwa mama Afrika anaweza kujitimizia matakwa ya teknolojia na maendeleo.

@JeremiahRotich,
Mkuu wa Mradi wa Swahilinux
profile

Swahilinux itakuwa msukumo kwa wengi na labda kurekebisha teknolojia barani Afrika ukizingatia kwamba muungano wa SADC unapania kuongeza Kiswahili kama lugha ya nne ya biashara na lugha ya kwanza ya kiasili ya Kiafrika.

@CharityIrungu, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano
profile

Swahilinux ni mfumo mbadala, tofauti na mifumo mingine iliyoundwa katika lugha za kigeni. Ni muundo unaolenga kuwezesha Waafrika kukumbatia Kiswahili na Teknolojia.

@BonareriSarah, Afisa Msaidizi Idara ya Mawasiliano
profile

Swahilinux ni mfumo wa aina yake uliovumbuliwa ili kukuza lugha ya Kiswahili. Je! Ni nani mwingine bora kukuza lugha yetu hii zaidi ya watu ambao wanatumia Kiswahili kwa mandhari ya kawaida? Swahilinux ni mfumo rahisi wenye ulioundwa kwa teknolojia ya kuaminika.

@GathoniMary, Wakili wa Swahilinux

Gumzo

Gumzo ni tovuti ya mawasiliano inayosimamiwa na Swahilinux Microsystems. Gumzo ni tovuti ya mawasiliano ya jamii ya Swahilinux ambapo mawasiliano na mipango yote yanatekelezwa. Mtu yeyote yule anaweza kujiunga; uwe msanifu, mtaalam wa maswala ya programu, mwanafunzi, n.k.
Jiunge na Swahilinux Gumzo leo

Jamii

Watu wote waliojiunga kwenye kundi zetu zozote au tovuti za mawasiliano zinazotambulika wanachukuliwa kuwa washiriki(wanajamii) wa timu zetu. Timu hizo zinasimamiwa na wasimamizi wa Swahilinux Microsystem (Timu ya Usimamizi wa Swahilinux). Ikiwa ungependa kuchangia katika mradi, wasiliana nasi kama ilivyoainishwa hapa chini.

Xiaoying Riley

Mahusiano ya Umma

Idara ya Mawasiliano

Ikiwa unataka kuchangia kwa kushiriki nasi maarifa yako ya uhusiano wa umma, upangishaji wa hafla na mikutano, blogi na maswala mengine ambayo hayahusiani na ustadi wa kutengeneza programu au tovuti, tutumie ujumbe kwa anwani zilizotajwa ili kutujulisha kile kinachoonekana kuwa cha kupendeza kwako.

Tom Najdek

Uvumbuzi na Ubunifu

Idara ya Uvumbuzi na Ubunifu

Ikiwa wewe ni mvumbuzi au mtu mbunifu ambaye ana maswali au suluhisho ambalo ungetaka kutoa kuhusiana na utaalam wowote wa programu, k.m. Teknolojia ya blockchain, akili ya kubuni (AI), uvumbuzi na ubunifu ya tovuti, usimamizi wa mfumo wa Linux, n.k. Wasiliana nasi kutumia kupitia anwani zilizotajwa hapo juu.

Wasiliana Nasi

Unaweza kuwasiliana nasi kupitia barua pepe au tovuti zilizoonyeshwa hapa

Tuma Barua Pepe